Jumanne , 29th Mar , 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Dodoma kutenga maeneo ya biashara ambayo ni rafiki kwa wafanyabiashara na yawe jirani na makazi ya watu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo

Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa manispaa hiyo ya kuhakikisha inalitoa ghala la ngozi lililopo makazi ya watu eneo la mailimbili Mjini Dodoma.

Mhe. Jaffo amesema uwapo wa ghala hilo kwenye makazi ya watu unahatarisha afya za watu hususani watoto kutokana na kutiririsha maji machafu huku akiutaka uongozi wa Manispaa hiyo kuwashauri wananchi kufungua biashara ambazo zinaendana na makazi ya Watu.

Kwa upande wake Kaimu Mkrugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Melkion Komba amemwambia Naibu waziri huyo kuwa wamtekeleza agizo lake na kuhakikisha kwa vitu vyote vilivyopo kwenye ghala hilo vimeondolewa.