.jpg?itok=jTw4Ou2w×tamp=1473626015)
Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamishna wa Jumuiya hiyo nchini Christos Stylianides amesema, msaada huo ni wapili na jumuiya hiyo ambapo kwa mara ya kwanza EU ilitoa paundi milioni 12.2 na kufanya msaada huo kufikia paundi milioni 22 tangu Aprili mwaka jana.
Christos amesema Tanzania imepokea wakimbizi wengi zaidi kuliko nchi za Rwanda, Congo na Uganda wakiwa na zaidi ya wakimbizi 140,000 na kupelekea kambi ya Nyarugusu Tanzania kuwa kambi kubwa zaidi duniani hivyo msaada huo utaiwezesha Tanzania kutoa huduma bora kwa wakimbizi hao.
Zaidi ya wakimbizi 260,000 nusu ya idadi hiyo wakiwa ni wanawake na watoto waliyakimbia makazi yao tangu mwezi Aprili mwaka jana kutokana na vurugu zilizovuka nchini Burundi kupinga uamuzi wa rais wa nchi hiyo Piere Nkurunzinza kugombea muula wa pili wa urais.