Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa Mataifa UNHCR limedai kwamba , Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kwamba taifa lake linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na lile la kifedha.
Ripoti hiyo anasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania.
Tanzania limekuwa eneo salama kwa wakimbizi wengi na sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wa Burundi ambao walitoroka mzozo na kwamba Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.
UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchii hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi.
Aidha Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa kinasema kuwa kinatuma ujumbe wa ngazi za juu kwa mazungumzo na serikali ya Tanzania.

