Alhamisi , 7th Apr , 2016

Kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazowakabili askari wa kulinda amani wa Tanzania nchini Congo DRC,Serikali imesema imechukua hatua dhidi ya askari hao ikiwamo uundwaji wa bodi ya uchunguzi.

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York, Balozi Tuvako Manongi.

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Balozi Tuvako Manongi,amesema suala hilo limemsikitisha Rais na Mkuu wa majeshi na kwamba wameshachukua hatua ikiwemo kuwazui wanajeshi hao wanaotuhumiwa kuto kutoka katika kambi walizopo nchini humo.

Aidhaa Balozi Manongi amesema kuwa hakutakuwa na hatua ya kurejeshwa kwa kikosi kizima nyumbani kufuatia tuhuma hizo kwa sababu ya wanajeshi wachache ambao wanatuhumiwa kufanya Unyanyasi huo.

Tuhuma hizo zinawakabili askari 11 wa Tanzania wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo DRC.

Sauti ya Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Balozi Tuvako Manongi,akizungumzia hatua walizochukua