Mtumiaji wa dawa za kulevya
Kongamano hilo liliitishwa na mamlaka ya kitaifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya nchini humo, ambapo ilishirikisha Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC nchini Tanzania.
Afisa mradi wa kitaifa wa mamlaka ya kitaifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya nchini , Immaculate Malyamkono ameeleza kile wanachojadili katika kongamano hilo ni pamoja na watumaiji wa dawa hizo kupata huduma za matibabu kama wengine ikiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi ya HIV pamoja na kupata dawa.
Bi. Malyamkono amesema mamlaka hiyo ya kitaifa au Drug Control and Enforcement Authority iliitisha kikao hicho ili Tanzania nayo iwe moja ya nchi zitakazokuwa na ajenda kuelekea UNGASS2016.
Aidha Mratibu huyo ameongeza kuwa tatizo la waathirika wa madawa ya kulevya kukosa huduma muhimu lipo kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi Tanzania ikiwa ni nchi moja wapo hivyo mojawapo ya mambo watakayojadili ni kujua ni jinsi gani wataweza kuwasaidia waaathirika wa madawa hayo.








