Jumatatu , 2nd Mei , 2016

Serikali imeanza kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda baada ya kuzindua ujenzi wa mradi maalum wa uwekezaji wa viwanda Mkoani Morogoro ili kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa vijana nchini.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,

Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katika eneo hilo maalumu lililopewa jina la Star City katika manispaa ya Morogoro.

Waziri Mwijage amesema wameamua kuanza na ujenzi katika Mkoa wa Morogoro kutokana na mazingitra na Jiografia yake kuwa nzuri kwa uzalishaji wa mazao tofauti.

Amesema Ujenzi wa viwanda katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa ya uwekezaji ni mpango wa serikali kuona inawatoa vijana kwenye kucheza pool,bao au kukaa vijiweni ili wajikite katika shughuli halai za uzalishaji