Alhamisi , 18th Feb , 2016

Shirika la afya ulimwenguni WHO na wizara ya afya ya Tanzania wanaandaa miongozo ya kusaidia kubaini iwapo kuna visa vya virusi vya zika nchini humo kama njia ya kudhibiti ugonjwa huo.

Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania Dkt. Janeth Mghamba

Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania Dkt. Janeth Mghamba amefafanua maeneo ambayo miongozo hiyo itajikita ni pamoja na kufuatilia takwimu za watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo pamoja na maeneo yenye mbu wa Aedes.

Dk Janeth pia amesema majaribio ya kubaini maamubukizi ya virusi vya Zika yatafanyika kuanzia wiki mbili kuanzia sasa na tayari wizara imeshaweka mpango maalum wa kuua sehemu za kuanzia kufanya utafiti wao.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa wanachukua hatua hizo baada kuonekana kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo ambapo kwa nchi za kiafrika umethibitishwa nchini Cape Verde.