Jumamosi , 14th Mei , 2022

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amewataka watanzania kuvitunza vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini, kwa maendeleo ya sasa na ya Baadaye.

Askofu wa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo

Askofu Shoo ametoa wito huo leo aliposhiriki katika mjadala kwa njia ya mtandao wa Zoom, Ulioandaliwa na Watch Tanzania News Agency huku akisisitiza kuwa utalii unauhusiano na mambo ya kiroho kwani humfanya mtu kuujua ukuu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

"Tanzania ni kama Paradiso, Tunaowajibu kiroho na kimaadili wa kuvitunza vivutio vyetu vya utalii, kwa ajili yetu na vizazi vijavyo" – Amesema Askofu KKKT Fredrick Shoo

Aidha Askofu Shoo amempongeza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kujitoa yeye mwenyewe kuvitangaza vivutio vya utalii nchini, akibainisha kuwa uwekezaji, biashara Tanzania.