Alhamisi , 1st Mei , 2014

Tanzania ndiyo nchi inayoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa wafanyakazi wake kukatwa kiasi kikubwa cha kodi kutoka katika mishahara yao, hatua inayowazidishia hali ngumu ya maisha.

Mjumbe wa kamati ya bunge ya uchumi, viwanda na biashara, David Kafulila.

Mjumbe wa kamati ya bunge ya uchumi, viwanda na biashara David Kafulila, amesema hayo leo wakati akitoa maoni kuhusiana na siku ya wafanyakazi ambapo amesema kiwango cha kodi katika mishahara kinaweza kupungua iwapo serikali itapunguza misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara.

Mbunge Kafulila, amesema kiwango cha misamaha ya kodi nchini Tanzania kimefikia asilimia nne ya pato la taifa wakati kiwango cha misamaha katika nchi nyingine ni asilimia mbili ya pato la taifa la nchi husika ambapo amesema kiwango cha kodi katika mishahara kinaweza kupungua iwapo serikali itapunguza misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara.