Jumatatu , 5th Mei , 2014

Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wahudumu wa fani ya ukunga ambapo takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa mkunga mmoja anahudumia takribani akina mama wajawazito mia tano.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe kwa Uzazi Salama (White Ribbon Alliance for Safe Motherhood), Bi. Rose Mlay.

Mkurugenzi wa mtandao wa utepe mweupe kwa uzazi salama Bi. Rose Mlay amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wakunga duniani na kufafanua kuwa kiwango hicho ni tofauti na viwango vya kidunia ambapo mkunga mmoja hutakiwa kuhudimia wajawazito sita.

Bi. Mlay ameongeza kuwa licha ya upungufu huo, bado mazingira wanayofanyia kazi wakunga hao hayaridhishi, kwani wengi wao hutoa huduma pasipo uwepo wa vifaa vya kutendea kazi na wakati mwingine hulazimika kufanya kazi kwa masaa zaidi ya saa ishirini.