Hayo yamebainishwa katika matembezi ya hiyari yakijumuisha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU,jeshi la polisi na kituo cha kutoa msaada wa kisheria cha Evarasting Kinondoni jijini Dar es Salaam yakiwa na madhumuni ya kuwaongezea uelewa wananchi kuhusu masuala ya rushwa hasa kwenye kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu.
Mchunguzi na mwendesha mashitaka TAKUKURU Bibie Msumi amewakumbusha wananchi kuwa kiongozi mzuri anapatikana pasipo na kutumia rushwa hivyo nijikumu la kila mtanzania kuhudhuria mikutano ya wagombea wote ili kumpigia kura kiongozi sahihi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kituo cha kutoa msaada wa kisheria cha Evarasting Hamis Masoud amesema kuwa bado jamii haina uelea wa kutosha kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria hivyo kwa kushirikiana na TAKUKURU na Jeshi la polisi kutawasaidia wananchi kutambua masuala ya kisheria hasa katika kipindi hiki.
Katika hatua nyingine TAKUKURU Kinondoni imewasihi wananchi kutoa taarifa wa taasisi hiyo endapo watapata taarifa au kuona kiashiria cha aina yoyote cha rushwa ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.





