Waziri wa Madini Anthony Mavunde
Ametoa maagizo hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo ambapo amesema mpaka sasa ujenzi wa kituo hicho cha afya umegharimu zaidi ya milioni 534 na inahitajika zaidi ya milioni 63 kukamilisha ujenzi wa mradi huo.
“Nimepita humu ndani mkuu wa mkoa kuna baadhi ya maeneo yalikosa usimamizi mzuri na wale wote ambao wamehusika TAKUKURU wamewachukulia hatua ninaomba nitoe maelekezo mkuu wa mkoa la kwanza ni kuhakikisha ndani ya wiki hii mtaalamu anatangaza tenda kwenye mfumo ili tumalizie fedha zilizobaki milioni 63 ili wananchi hawa waanze kupata huduma katika kituo chao cha Afya” Anthony Mavunde-Waziri wa Madini.
Akisoma taarifa ya mradi huo Afisa mtendaji wa kata ya ushirika Juma Luchagula amesema kituo hicho kitakapokamilika kitahudumia zaidi ya wananchi elfu 35.