
Wagombea wote waliopitishwa na kamati wanaweza kuanza kampeni kuanzia Machi 27 na Mkutano Mkuu utafanyika Mei 11-13, 2023 jijini Arusha
Taarifa ya TLS imesisitiza kuwa Wakati wote wa kampeni wagombea wote kufanya kampeni za kistarabu kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi za chama.
Hata hivyo imeeleza kuwa wale wote ambao hawajarizishwa na maamuzi ya kamati ya uchaguzi, wanatakiwa kukata rufaa kwenye Electoral Appeals Committee kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo