Jumatano , 4th Oct , 2023

Kevin McCarthy ameangushwa katika uasi wa mrengo wa kulia - ikiwa ni mara ya kwanza kwa spika wa bunge la Marekani kupoteza kura ya kutokuwa na imani naye. 

Kura ya mwisho ilikuwa 216-210 kumuondoa mbunge huyo kama kiongozi wa walio wengi wa Republican katika bunge la chini la Congress.

Watu wenye msimamo mkali katika chama chake walipiga kura dhidi yake baada ya kufikia makubaliano na Democrats wa Seneti kufadhili mashirika ya serikali.

Hakuna mrithi wa wazi wa kusimamia wingi wa wabunge wa Republican.

Bunge la Congress lina zaidi ya siku 40 za kukubaliana juu ya mpango wa kuzuia uwezekano mwingine wa kufungwa kwa serikali.

Mrepublican wa Florida Matt Gaetz, mshirika wa Trump, aliwasilisha chombo cha kiutaratibu ambacho hakitumiki sana kinachojulikana kama hoja ya kumfukuza bwana McCarthy Jumatatu usiku.

Alimshutumu Spika kwa kufanya makubaliano ya siri na Ikulu ya White House kuendelea kufadhili Ukraine, huku kukiwa na mazungumzo ya kuzuia kufungwa kwa serikali mwishoni mwa wiki. Bwana McCarthy alikanusha madai hayo.