Jumatano , 26th Apr , 2023

Serikali kupitia Shirika la Masoko ya Kariakoo limesema ukarabati wa soko hilo umefikia asilimia 85 huku likitarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi wa 10 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa soko hilo Mwenyekiti wa Shirika La Masoko Ya Kariakoo Hawa Ghasia amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo kutaleta nafuu kwa wafanyabiashara wengi na tayari wafanyabiashara 1400 kati ya 1662 wameshahakikiwa.

Nae Meneja Mkuu Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Kaijage amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi pamoja na ukarabati wa soko kuu la kariakoo unatarajiwa kuzalisha ajira 4000 kwa watanzania.