Patrick Mususa
Limesema kuwa mwenendo wa soko unatokana na msukumo wa nguvu ya soko ya uhitaji na uuzaji wa hisa.
Meneja Miradi na Biashara wa Soko hilo Bw. Patrick Mususa amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa mwelekeo wa soko katika kipindi cha wiki moja iliyopita ambapo mauzo ya hisa sokoni hapo yamepanda kwa takribani mara 9 kutoka mauzo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 shilingi 16.2 bilioni.
Aidha, Mususa amesema katika kipindi hicho, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepanda kwa zaidi ya mara 14, kutoka hisa 347,147 hadi hisa milioni 4.8 huku ukubwa wa mtaji wa soko ukiongezeka kwa asilimia 3.9 kutoka shilingi trilioni 20.8 hadi shilingi trilioni 21.6.