Jumamosi , 17th Feb , 2018

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria  Mhe. Muhidin  Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Slaa leo wamekutana na Makamu wa Rais , Samia Suluhu  kwenye makazi yake Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo

vyao vipya vya kazi.

Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Ikulu jijini Dar Es Salaam, Mh. Suluhu amewatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais.

Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji  ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” amesema Mh. Suluhu

Kwa upande wao Mabalozi hao wamemuahidi Makamu wa Rais  kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.