Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sisi hatuna vurugu, Haki itendeke - Elvis

Jumamosi , 17th Feb , 2018

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha (CHADEMA) Elvis Mossy amefungukia matamko yanayotolewa ya kuhusu kupiga kura na kwenda nyumbani ambapo amesema kwamba matamko hayo yanakinzana kanuni ingawa ametaka haki itendeke kwani wananchi wake siyo watu wa vurugu

Akizungumza akiwa kata ya Engarenairobi huko Siha mkoani Kilimanjaro, Mossy amesema kwamba kanuni zinahitaji watu wajae mita 100 baada ya kupiga kura lakini kama haki itatendeka wananchi wa Siha hawatakuwa na haja ya kulinda kura.

"Hatuna vurugu sisi. Kama wanataka turudi majumbani tutaenda tu. sisi tunachotaka ni haki, akishinda Mollel atangazwe lakini nikishinda mimi nitangazwe. Ila Kailima anajua kwamba kanuni zimeweka wazi mpiga kura anapaswa kukaa mita kadhaa baada ya kupiga kura" Elvis

Akizungumzia changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza, Mossy amesema kwamba mawasiliano yamekuwa kikwazo kikubwa kwani fomu za kura zimekuwa chache katika moja ya kituo lakini Mkurugenzi hapokei simu ili kuweza kutatua changamoto hiyo.

"Mawasiliano ni changamoto ya kwanza, Mkurugenzi wetu wa hapa hapokei simu lakini nimemwambia Kailima ameahidi kutusaidia. kuna kituo kina fomu 60 na wakati zinahitajika kama 400" .

Mbali na hayo taarifa mbalimbali zinasema katika jimbo la Siha watu mbalimbali wamejitokeza kupiga kura huku eneo la Sanya Juu wazee wakionekana kuwa wengi kuliko vijana.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea