Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Utafiti wa shirika lisilo la kiserikali la Sikika nchini Tanzania unaonyesha kwamba zaidi ya vituo elfu 5 vinavyotoa huduma ya afya kwa umma, havina dawa muhimu na hivyo kusababisha wananchi wanaofika katika vituo hivyo kukosa huduma.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Irinei Kiria amesema katika vituo hivyo walivyovifanyia utafiti wamegundua hali ya upatikanaji wa dawa muhimu ni mbaya.

Kwa mujibu wa Kiria, Sikika inawasihi wabunge kuishauri serikali kuongeza bajeti ya wizara ya afya ili kutatua tatizo hilo wakati huu ambapo bajeti ya wizara hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni siku yoyote wiki hii.