
Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Kunduchi Michael Urio amesema mpaka sasa wamelazimika kufunga shule hiyo ya Watoto ya mchepuo wa kiingereza kutoendelea na masomo kwa wanafunzi kwa sababu za kiusalama ambapo ameiomba TANROADS kusaidia kujenga mitaro itakayosaidia kutoa maji katika maeneo hayo
Urio amesema kama ambavyo miradi mwingine inapewa kipaumbele kama vile barabara na madaraja basi swala la elimu pia lipewe kiupaumbele
Shule ya Msingi Michael Michael Urio ina wanafaunzi zaidi ya mia nane ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi 500 wameandikishwa ambapo zaidi ya wanafunzi 900 watakosa kwa kuwa shule hiyo itafungwa mpaka mazingira yatakapokuwa Salama