Jumamosi , 18th Jul , 2020

Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa amewatoa hofu wamiliki wa shule jijini humo na kuwa wameunda timu inayofanya uchunguzi kuhusu matukio ya moto ambayo yametokea katika shule tatu katika eneo la Kinondoni.

Mabaki ya vitu vilivyoungua katika moto uliotokea katika shule ya Sekondari ya Mivumoni Kinondoni Dar es Salaam

Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa amewatoa hofu wamiliki wa shule jijini humo na kuwa wameunda timu inayofanya uchunguzi kuhusu matukio ya moto ambayo yametokea katika shule tatu katika eneo la Kinondoni.

SACP Mambosasa ameyasema hayo baada ya kufika katika Shule ya Mivumoni Islamic ambayo moja ya madarasa yake yameungua moto ikiwa ni tukio la pili kutokea baada ya siku moja Shule nyingine ya Kinondoni Muslim kuungua kwa moto.

“Tumetoka katika janga la Corona na wanafunzi hawa wameanza masomo yao hatuwezi kufumbia macho ya matukio kama haya ni lazima tuyafuatilie kwa kina” amesema Mambosasa.

Aidha Mambosasa ametoa wito kwa taasisi zikiwemo shule na maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu kuhakikisha wanakuwa na vifaa muhimu kwaajili ya kuzima moto endapo majanga kama hayo yatatokea ili kuokoa mali.

“Kinga mara zote ni bora kuliko kutibu kwahiyo kujiandaa na majanga ni jambo zuri sana ili kusaidia madhara hayo jititahidi kupata elimu kutoka kwa watu wazimamoto”