Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan,
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa chanzo cha uharibifu huo ni pamoja na ukataji miti hovyo shughuli za kibinadamu ikiwemo Kilimo,Ufugaji na uchumbaji wa madini.
Mhe. Suluhu amesema hali hiyo imepelekea kupungua kwa mtiririko wa maji katika mito mingi nchini kwa kipindi cha miongo mitano iliyopita na kusema endapo hali hiyo itaendelea basi mito mingi itakauka ndani ya miaka 15.
Mhe Samia ametumia nfasi hiyo kuitaka jamii kushiriki kikamilifu kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kupanda mti kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo hivyo na kupiga marufuku zote za kibanaadamu.
Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi amesema kuwa watanzania wengi hasa walio katika maeneo ya vijijini na mijini hawana elimu ya kutosha juu ya uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi amesema hakuna maendeleo ya kiuchumi yanayoweza kupatikana kama elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira haitaweza kuwafikia watanzania wengi zaidi.