Jumapili , 27th Jan , 2019

Vyama 10 vya Upinzani nchini wameipongeza Kamati ya Bunge kwa kuweza kubadili baadhi ya vifungu ambavyo walivizungumzia hapo awali katika mapendekezo ya muswada wa sheria ya vyama vya siasa nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam wamepongeza hatua ya kuondolewa kwa hati yenye mashaka kama kigezo cha chama kusitishiwa ruzuku na kuongeza kuwa bado muswada huo unahitaji marekebisho zaidi ikiwemo kupunguzwa kwa ujinai.

"Haya mambo yana sheria zake, tuyaache yashughulikiwe na sheria zake ili kufanya siasa nchini Tanzania isigeuke kuwa jinai", amesema Naibu Katibu Mkuu CHADEMA bara.

Aidha amewaasa wabunge wa CCM kufuata nyayo za wenzao walio kwenye Kamati ya Katiba na Sheria katika kuweka maslahi ya nchi mbele pindi Muswada utakaposomwa mara ya pili na kujadiliwa.