Akiongea katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam Dkt Hamza Khalifa Kondo ambaye pia ni mwandishi wa habari amewataka wanahabari kupigania sheria zote kandamizi kwa uhuru wa habari zifanyiwe marekebisho ili kuongeza hadhi ya tasnia hiyo ambayo ni muhimili wanne wa dola.
Aidha Dkt Hamza amesema utafiti unaonesha kuwa sheria kandamizi kwa uhuru wa habari ziko 24 licha ya kuwa ni sheria mbili pekee ndizo zinazungumziwa jambo ambalo linatishia uhuru wa tasnia ambapo ametaka kuundwa kwa bodi ya wataalam ili kusimamia masuala ya habari.
Dkt Hamza amesema ni vyema serikali ikatekeleza makubaliano ya umoja wa mataifa inayosisitiza uhuru wa habari kwa kuweka kisheria kwani ni haki ya msingi kwa mtu kupata habari.







