Picha ya ukumbusho wakati Mwl. Julius Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar ishara ya Muungano.
Majaliwa ameyasema hayo leo April 25, 2019 ofisini kwake jijini Dodoma, ambapo ameweka wazi kuwa kesho ni siku ya mapumziko ya kitaifa lakini hakutakuwa na sherehe za kitaifa.
Aidha Majaliwa ameongeza kuwa fedha kiasi cha sh. milioni 988.9 zilizokuwa zitumike kwenye sherehe hizo, zimeokolewa na zitapangiwa matumizi mengine.
Tanzania kesho inaadhimisha miaka 55 tangu nchi za Zanzibar Visiwani na Tanganyika ziungane mwaka 1964, chini ya viongozi wa wakati huo Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.