Ijumaa , 19th Feb , 2016

Serikali ya Tanzania inakusudia kupanga, kupima,kumilikisha na kusajili kila kipande cha ardhi nchini kwa lengo la kupunguza migogoro ya ardhi ambayo inapelekea usumbufu mkubwa kwa watanzania.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.William Lukuvi (Katikati)

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.William Lukuvi ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwezesha umilikishaji ardhi nchini kwa lengo la kutuma na kusimamia utekelezaji wa sheria mbalimbali katika sekta ya ardhi ambazo zimekubalika kuwa miongoni mwa sheria bora katika nchi zinazoendelea.

Waziri amesema hatua hiyo itasaidia kuepusha wawekezaji wakubwa katika ardhi kuchukua maeneo makubwa ya ardhi bila kujali maslahi ya wanakijiji kama ilivyo katika maeneo mengine duniani.

Programu hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 15.2.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe amesema mpango huo utasaidia kuondoa migogoro na kuwapa wananchi fursa ya kumiliki ardhi ambayo wataweza kwenda benki kuchukua mikopo na kuinuka kiuchumi

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kilombero Peter Lijialikali amesema kuwa utarartibu huu ulioanzishwa na serikali utasaidia kuleta majibu yakuondoa migogoro ya Ardhi nchini