Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 16, 2023, kufuatia kukamatwa kwa Balozi Dkt Willbrod Slaa, Mdude Nyagali pamoja na Wakili Boniface Mwabukusi, ambapo Waziri Nape amesema watu hao wamekamatwa kutokana na kauli zao zinazoashiria vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na kupanga maandamano ya kuiondoa serikali madarakani.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kwamba tangu serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ilipoingia madarakani imekuza demokrasia pamoja na kuruhusu mikutano ya hadahra kwa vyama vya siasa pamoja na uhuru magazeti na TV za mtandaoni zilizokuwa zimefungiwa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa serikali itaendelea kuacha kila mtu kuwa na uhuru wa kujieleza iwe kwa njia ya mtandao ama nyingine katika mijadala mbalimbali yenye kulenga mipango ya maendeleo ya nchi na mambo mengine yenye maslahi kwa Taifa.