Ijumaa , 17th Nov , 2023

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kifo cha Mtanzania Clemence Felix Mtenga ambaye ni mmoja kati ya watanzania wawili pamoja na raia wa mataifa mengine waliokuwa hawajulikani walipo tangu yaliyopotokea mapigano Oktoba 7, 2023 nchini Israel

Majengo yaliyoporomoka kutokana na mashambulio

na katika maeneo ya Wapalestina hususani Gaza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara imesema Clemence alikuwa ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo kuijulisha familia na inaendelea kuwasiliana na serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi zinakamilika kwa wakati.

Wizara imesema inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo “Wizara inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu”