Vijana wakiwa wamejumuika katika kuvuta Shisha
Akizungumzia katika mahojiano maalumu na East Africa Radio hii leo Bi. Kagaruki amesema kuwa licha ya serikali kutoa tamko la kupiga marufuku matumizi ya bidhaa hizo lakini pia inatakiwa kurekebisha sheria ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku ili tamko hilo liweze kutekelezeka kisheria.
Bi. Kagaruki ameongeza kuwa takwimu za matumizi ya tumbaku dunia zinatishia uhai wa kizazi kilichopo ambao kwa ripoti iliyotolewa mwaka huu kuwa tumbaku inaua watu milioni 6 kwa mwaka kwa wanaotumia huku watu laki 6 wakifariki duni kwa kuvuta moshi wa tumbaku pasipo kutumia moja kwa moja.
Ameongeza kuwa vijana wengi walijiingiza kwenye matumizi ya tumbaku hasa uvutaji wa sigara lakini takwimu haikuwa kubwa kama ambavyo utumiaji wa tumbaku wa aina nyingine unajulikana kama shisha umeongeza ukubwa wa athari za tumbaku kwa jamii nchini hususani vijana.

