
Catherine ameyasema hayo alipokuwa akiuliza maswali Bungeni ambapo swali la Msingi kuhusu vijana ni swali la Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aliyeuliza mpango wa serikali katika kutengeneza ajira kwa vijana ili wasikubwe na adhabu kwa kukaa mtaani na kucheza pool table.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde Ili kuhakikisha hakuna vurugu kati ya vijana wasio na ajira na makundi mbalimbali, Serikali inatekeleza mpango wa maendeleo wa pili wa miaka mitano 2016/17- 2020/21 ambapo umejikita zaidi katika kukuza viwanda vidogo na vya kati.
Akiuliza swali la nyongeza Bi. Magige ameiuliza serikali isiwape vijana wa Arusha kwa kuwa msemaji wao Godbless Lem hayupo Bungeni ili uchaguzi ujao CCM iweze kupata kura nyingi zaidi.
Naibu Waziri Mavunde akijibu swali hilo amesema ''Nataka niwaondoe hofu wananchi na vijana wa Arusha kwa kuwa yule waliyemchagua hayupo Bungeni lakini serikali hatutawabagua tutahakikisha wanapata mafunzo na mitaji ya kujiendeleza''