Jumatano , 6th Jul , 2016

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kushirikia katika uvunjifu wa amani.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kushirikia katika uvunjifu wa amani na utulivu kupitia itikadi za kidini na kisiasa.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za Iddi el Fitri zilizofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kusheherekea siku hii kwa kuwatembelea wale wasiojiweza pamoja na kudumisha amani na ushirikiano kama ilivyokuwa katika kipindi cha mfungo wa siku 30.

Kwa upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zuberi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kote nchini kutumia siku ya leo kwa ajili ya kuwasaidia masikini na yatima pamoja na kudumisha amani na mshikamano.