Ijumaa , 4th Sep , 2015

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema wakati Tanzania inajiandaa kutekeleza awamu ya pili ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016 -2020) ambao unalenga kukuza viwanda nchini, haina budi kuangalia ni aina gani ya uwekezaji unafaa kuchukuliwa.

Waziri Mkuu wa Jamahri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda

Pinda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mabalozi na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 70 ya uhuru wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na miaka 50 ya kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Vietnam, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri mkuu Pinda alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka makampuni ya Ki-Vietnam waje kuwekeza nchini kwenye usindikaji wa korosho, utengenezaji wa saruji na viwanda vya nguo.

Aliyataja maeneo mengine ambayo wenye makampuni wanaweza kuwekeza kuwa ni nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ujenzi wa nyumba za kuishi.