Waziri Muhagama ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam katika kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji,kongamano ambalo limehusisha nchi zaidid ya tano duniani kwa lengo la kuhakisha linaweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza pato la taifa.
Waziri amesema mikakati ya serikali ni pamoja na kuhakikisha kuwa makampuni ya gesi na migodi mikubwa yanaongeza kiwango cha manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini kwa lengo la kuongeza soko la bidhaa za ndani sambamba na kufanya tathmini za kina ili kufahamu uwezo na mapungufu yaliyopo hasa masuala ya uwezeshi wa mitaji na ajira kwa vijana na tayari serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kuwawezesha vijana.
Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Dr. Reginald Mengi amesema watanzania wapewe nafasi ya kwanza katika sekta ya uwekezaji kwakuwa kuna watanzania wengi wanauwezo wakuwekeza katika masuala ya uchuni.
Naye mkurugenzi wa baraza la uwekezaji nchini NEEC Bein'g Issa amesema kuna fursa nyingi zinazotokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea hapa nchini katika sekta ya gesi, mafuta,migodi na ujenzi.




