Jumapili , 30th Oct , 2016

Wizara ya afya imeaanza kutoa chanjo ya saratani ya majaribio mkoani Kilimanjaro, kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 9 hadi kumi na tatu ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa saratani kwa wanawake hasa ya mlango wa uzazi na saratani ya matiti

Naibu Waziri wa Afya Mh Hamisi Kigwangwala

Akizungumza jijini Arusha na waandishi wa habari wanawake naibu waziri wa afya Mh Hamisi Kigwangwala, amesema iwapo chanjo hiyo ya majaribio itafanikiwa kwa kiwango kikubwa itatolewa nchi nzima, na kuwa itawafanya wanawake wa kitanzania kuwa salama.

Aidha Dr Kigangwala amesema ili kujiondoa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huo, wanawake wanapaswa kujiepusha na kujamiana na wanaume wengi hali inayoelezwa kuwa inaongeza hatari ya kukutwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Daktari anahusika na matibabu ya saratani katika hospitali ya Mount Meru Mwanahamis Gembe, amesema kwa sasa mwamko wa wakinamama wa kujitokeza kupima ni mdogo ikilinganishwa na idadi ya wanawake wa mkoa wa Arusha.

Licha ya ukubwa wa tatizo inaelezwa kuwa wakinamama hasa wa maeneo ya vijijini kwa asilimia 50 hawana ufahamu wowote kuhusu ugonjwa huo.