Msajili wa Hazina amesema Serikali imeshapeleka wataalamu wa kibenki kushugulikia tatizo lililopo kwa sasa katika Benki ya Twiga Bancorp kuhakikisha watanzania hawapotezi fedha zao.
Hayo yamesemwa na msajiri wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru wakati akitolea ufafanuzi jambo hilo ikiwa Tanzania inaelekea siku ya maonyesho ya kibenki nchini, na kusema kuwa serikali haiwezi kuendelea kuwekeza kwenye Benki hiyo na tayari wanafanya mikakati mingine ambayo itawezesha kubadilisha dhamana zake kwa mabenki mengine.
Mafuru ameongeza kuwa katika kuhakikisha mabenki mbalimbali nchini yanafanya shughuli zake za kibenki kwa taratibu zilizowekwa ili zishiriki katika kukuzaa uchumi wa nchi.
Kwa upande wake msimamiazi wa siku za kibenki na taasisi zake nchini Bwana Leo Nyanduga amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo katika kujifunza zaidi shughuli za kibenki.









