Jumatatu , 28th Sep , 2015

Tanzania inatarajia kupata miradi ya uwekezaji itakayoliingizia taifa zaidi ya Dola za Marekani milioni 1000 katika sekta za utalii na uhifadhi nchini ikiwa ni awamu ya pili ya mkakati wa uwekezaji nchini katika Sekta hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji nchini(TIC), Juliet Kairuki

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji nchini(TIC), Juliet Kairuki iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana makakati wa uwekezaji katika miradi hiyo ulipitishwa September mwaka huu chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezekezaji(NISC).

Kairuki ameongeza kuwa uwekezaji huo ni kutoka nchini Marekani ikiwa ni matokeo ya juhudi za Rais Kikwete kufungua milango ya Wawekezaji nchini kwa wawekezaji kutoka nchi hiyo na nyingine.

Aidha amesema kuwa ujio wa uwekezaji huo utasaidia kuongeza ajira, uhifadhi wa wanyamapori, maendeleo ya Sekta ya Utalii, Maendeleo ya Wananchi wanaozunguka maeneo ya utalii, uboreshaji wa maeneo ya vivutio vya uwekezaji na nchini na kufungua maeneo mapya ya uwekezaji.