Mgombea Urais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Akiongea na waandishi wa habara jana mara baada ya uchaguzi huo kuahirshwa Maalim Seif amesema kuwa kwa mujibu wa waangalizi wa kimataifa wametoa tathmni yao juu ya uchaguzi huo na kusema ulikuwa huru na wa haki hivyo tume ya usimamizi visiwani humo itoe matokeo ya mshindi visiwani humo.
Aidha Maalim Seif amtoa wito kwa viongozi wa pande zote husika kukaa chini na kutafuta suluhu ya suala hilo huku akiwataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo hasa kwa kipindi hiki.
Kwa upande wake mgombea wa urais wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mh, Edward Lowassa ametangaza kutokubaliana na mtokeo yanayotolewa kwa sasa na tume huku akiitaka tume hiyo kuacha kutangaza matokeo hayo haraka.
Mh. Lowassa amesema kuwa katika maeneo mengi ambayo tume imetangaza matokeo hayo inaonekena yamechakachuliwa hivyo hawezi kukubaliana na matokeo hayo kwa kuwa yanaonekana dhahiri kumbeba mgombea wa chama tawala Dkt. John Pombe Magufuli.