Samia kuhutubia Bunge la Kenya 

Jumapili , 2nd Mei , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumanne ya Mei 4, 2021, ataanza ziara ya siku mbili nchini Kenya na atakutana na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na moja ya majukumu atakayoyafanya ni kuhutubia Bunge la Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Taarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, na kusema kuwa pia katika ziara hiyo atazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano na ushirikiano kati ya nchi ya Kenya na Tanzania kwa lengo la kuuimarisha na kuuboresha zaidi.

"Bunge hili litajumuisha mabunge yote mawili, pia Mei 5 atahudhuria jukwaa la wafanyabiashara wa pande zote mbili, hivyo imempendeza kuhutubia katika jukwaa hilo na kuzungumza na wafanyabiashara wa pande zote mbili na kuwaeleza fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania na maeneo ambayo wanaweza kuja kufanya biashara na kuwekeza", ameeleza Msigwa.

Mara baada ya ziara hiyo Rais Samia atarejea nchini kwa ajili ya kundelea na majukumu yake.