
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson.
Wakiongea nje ya Bunge hilo baadhi ya wabunge hao wa upinzani wamesema Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia ameshindwa kuongoza bunge kwa maslahi ya wananchi kwa kuwa suala hilo limewaathiri vijana wengi hasa watoto wa kike.
Akiongea na waandishi wa Habari Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) Mhe. Joshua Nassari amesema Naibu Spika ameshindwa kutumia busara kuzuia suala hilo kujadiliwa wakati watoto wengi hawana kwa kwenda na wala hawajui hatma yao.
Kwa upande wao baadhi ya wabunge wa Chama Tawala CCM wameunga mkono hoja iliyotolewa na Mhe. Joshua Nassiri akiwemo Mhe. Kangi Lugola pamoja na Stenslaus Mabula wamesema suala hilo ni zito ambalo serikali inahitaji kuchukua hatua za haraka.
Wabunge hao wamesema ni jambo lisilokubalika kufukuzwa kwa wanafunzi hao ambao walipelekwa chuoni hapo kwa utaratibu maalum wa kuweza kuwasaidia watoto hao kusoma masomo ya Sayansi ili kupunguza tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi nchini.