Alhamisi , 20th Nov , 2014

Wabunge Bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelitaka Bunge kuachana na Barua ya mahakama inayotaka kuzuia sakata la Kashfa ya fedha katika akaunti ya Tegeta ESCROW lisijadiliwe na kutolewa maamuzi Bungeni kwa kuwa liko Mahakamani.

Wabunge Bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelitaka Bunge kuachana na Barua ya mahakama inayotaka kuzuia sakata la Kashfa ya fedha katika akaunti ya Tegeta ESCROW lisijadiliwe na kutolewa maamuzi Bungeni kwa kuwa liko Mahakamani.

Wakitoa ushauri kwa Bunge na Kamati ya Uongozi, Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe. Davidi Kafulila amesema mahakama imekosa uhalali na mamlaka ya kisheria na kikanuni ya kuzuia Bunge kuendelea na utaratibu wake katika kufuatilia sakata la ESCROW.

Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala CCM wamelitaka Bunge kuchukua hatua katika hilo kwa kuhakikisha taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali kuhusu wizi huo wa mabilioni ya fedha iwasilishwe bungeni.

Kwa upande wao wabunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wametaka Barua hiyo kuwekwa mezani ili kuliwezesha Bunge kumjadili kiongozi wa mahakama kama hoja mahususi kwa mujibu wa kanuni ya 64.1(e) ambaye amediriki kuingilia mamlaka ya Bunge na kulifundisha kazi zake.

Akielezea kwa ufupi hatua ya kamati ya PAC inayochunguza sakata la ESCROW ilipofikia mwenyekiti wa kamati ya PAC amependekeza kuwepo kwa mjadala ili kuweza kuondoa Minong’ono pamoja na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.

Aidha akizungumzia sakata hilo, Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda amependekeza katika kutatua sakata hilo ni lazima Bunge litumie Busara kubwa ili kuahikikisha maamuzi yatakayotolewa hayataleta hisia za muingiliano wa majukumu na mahakama.

Tags: