Jumatatu , 19th Aug , 2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema sakata la binti aliyedhalilishwa kwa kubakwa lazima haki itatendekea na kuwataka wananchi kuwa na uvumilivu

Dkt.  Gwajima amesema hivyo baada ya mitandao mbalimbali kuandika kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC mkoa wa Dodoma juu ya salata hilo

Kupitia taarifa fupi aliyoiweka kwenye mitandao yake ya kijamii Wazimaoni juu ya sakata hilo 

"Ndugu Wananchi, nimepokea 'Tags' nyingi za maoni na maswali kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC mkoa wa Dodoma juu ya mwenendo wa shauri la 'Binti wa Yombo' (rejea taarifa za awali)"

"Ndugu Wananchi, nimepokea hisia zenu, maoni na maswali yenu ambayo mmeelekeza kwangu. Nimewasiliana na Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye tayari naye amepokea na anafanyia kazi hivyo, tumpe nafasi atatoa taarifa yake"

"Ndugu Wananchi, ni dhahiri kuwa, alichofanyiwa 'Binti wa Yombo' ni kitu kibaya kisicho cha utu hivyo, anastahili haki yake kwa mapana yote. Ndugu Wananchi, Nawasihi tujipe muda na kuamini kuwa, haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na siyo vinginevyo" amesema Waziri Dkt. Dorothy Gwajima kupitia mitandao yake ya kijamii