Jumatano , 4th Aug , 2021

Kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake, imeshindwa kuendelea hii leo Agosti 4, 2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, baada ya Sabaya kushindwa kufika mahakamani hapo kwa sababu za kiafya.

Lengai Ole Sabaya, akiwa na wenzake mahakamani siku za nyuma

Shauri la kesi hiyo limeahirishwa na Hakimu Mwanamizi Mkazi wa Mahakama hiyo Odira Amworo, na kusema kuwa kesi hiyo itaendelea tena hapo kesho Agosti 5, 2021, kwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi namba 7 ASP Gwakisa Minga ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wilaya ya Arusha.