Mabaki ya ndege iliyoanguka
Rubani wa ndege hiyo anasikika katika mkanda huo wa video akiomba ruhusa kutaka kutua kutokana na hitilafu ya umeme na kutokuwa na mafuta.
Wachezaji wa klabu ya Chapecoense, walitarajiwa kushiriki katika mpambano wa fainali huko Medellin mchezo ambao ungechezwa jana jioni dhidi ya timu ya Atletico Nacional lakini mashabiki wa soka walifurika katika uwanja huo kuomboleza na kutoa heshima zao za mwisho.

Mashabiki wa Atletico Nacional waliofurika uwanjani kuomboleza
Maelfu ya waombolezaji walionekana wakiwa na mishumaa na wakiwa wamevaa mavazi meupe.









