Jumatano , 5th Jan , 2022

Wazazi na wa mwanafunzi wa kike (15) aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kolero wilauani Morogoro, wamelilalamikia jeshi la polisi kushindwa kumchukulia hatua mwalimu anayetuhumiwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo huku akiendelea kutamba kijijini hapo.

Mwanafunzi aliyepewa ujauzito na mwalimu wake

Akizungumzia namna tukio hilo lilivyotokea mwanafunzi huyo amesema kuwa chanzo cha hayo yote ni mwalimu kuchukua saa ya mwanafunzi huyo na kisha baadaye alimuomba urafiki na kuanza kumletea zawadi kidogo kidogo na ndipo mazoea yao yalipozidi.

Akisimulia zaidi mwanafunzi huyo amesema, mwalimu huyo alimuahidi kwamba angemsaidia katika masomo yake na kwamba angemuoa ila baada tu ya kumpa ujauzito hajawahi kumsaidia kwa chochote.