Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini RITA imewataka wanafunzi hasa wanaotarajia kufanya maombi ya kujiunga na vyuo vikuu ama kupatiwa mikopo kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya Vifo vya wazazi wao Kupitia E huduma kwa njia ya Mtandao popote walipo.
Kauli hiyo imetolewa meneja masoko na mawasiliano kutoka RITA bw Josephat Kimaro ambaye amesema kupitia huduma mpya ya E HUDUMA kwa Sasa wananchi wanauwezo wa kusajili maombi ya vyeti vya kuzaliwa au kifo kwa njia ya mtandao popote waliko Tofauti na ilivyokuwa huko awali.
Amesema Lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kufanya Maboresho yaliyolenga kumpunguzia mwananchi Gharama Ambapo kwa Sasa mwitikio umekuwa mkubwa kutoka na na kuwepo kwa zaidi ya maombi 6000.
Bw Kimaro amesema kuanzishwa kwa E -huduma kumeondoa changamoto ya awali iliyokuwepo ya mtu kusajili akiwa akiwa katika Wilaya aliyozaliwa.





