Alhamisi , 11th Mei , 2023

Taarifa za Jeshi la polisi nchini Ujerumani zimesema Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi kwenye kiwanda cha Mercedes Benz nchini Ujerumani.

Mshukiwa amezuiliwa baada ya kupigwa risasi huko Sindelfingen, polisi katika mji wa karibu wa Ludwigsburg wamethibitisha taarifa hizo

Kikosi hicho hapo awali kiliandika kwenye Twitter: "Kwa sasa kuna operesheni ya polisi kwenye eneo la kiwanda. Polisi na waokoaji wako kazini na kwamba hakuna hatari kwa idadi ya watu ambao wanaendelea na kazi

Mercedes Benz imethibitisha kuwa tukio limetokea huko Sindelfingen na inawasiliana na mamlaka.

Kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba wamewasiliana na mamlaka na kueleza kwa kina ukweli wa tukio hilo na kwamba Usalama wa wafanyikazi ndio kipaumbele chao.