Ijumaa , 30th Sep , 2022

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime, amewataka Watanzania kurudi kwenye misingi ya imani za dini na kuachana na uhalifu hatua ambayo itaepusha matukio ya washukiwa wa uhalifu kupigwa risasi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 30, 2022, kupitia mjadala uliofanyika kupitia mitandao ya kijamii wakati akijibu swali lililouliza sababu zilizopelekea vijana waliokamatwa kwa tuhuma za panya road kupigwa risasi kwenye makoromeo.

"Kwa ufupi tu kwamba wakati wa mapambano risasi haichagui sehemu ya kuingia, sehemu yoyote inaweza kukupata, cha msingi Nondo atusaidie kwa vijana wenzake awape elimu kurudi kwenye misimamo ya dini zetu kuacha dhambi ambayo sisi polisi tunaiita ni uhalifu, turudi kwenye msimamo wa kuchukia uhalifua kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa," amesema SACP Misime