Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini CAG Prof. Mussa Assad
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema katika ripoti yake wamegundua taasisi za Serikali na vyama vya siasa vikipata kasoro chache kwenye matumizi yao ya pesa.
"TRA ina kesi za kodi zenye thamani ya shilingi Tril. 382.6 kwenye mamlaka za rufaa za kodi, sawa na ongezeko la shilingi Tril. 378.2 ikilinganishwa na 2016/17, ongezeko limechangiwa na mashauri 4 yanayoihusu Kampuni ya Uchimbaji Madini ya ACACIA", amesema Prof. Assad.
"Tumewaalika wenyeviti wa Kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa, tutawapatia nakala hizi", ameongeza Prof. Assad.
"Kati ya majalada 2,868 ya malipo ya mafao yaliyokaguliwa 2017/18, mafao ya wastaafu 295 yalikokotolewa kimakosa, majalada 172 yamebainika kuwa na ziada ya malipo ya shilingi Mil. 577, majalada 123 yakiwa na upungufu wa malipo wa shilingi milioni 294" amesema Prof. Assad.
April 2, 2019 Bunge la Tanzania lilifikia azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Prof Mussa Assad kwa kutoa kauli kuwa Bunge ni dhaifu.








