
Mhe. Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa Geita Vijijini
Wabunge hao wamechukua hatua hiyo leo Aprili 5, 2022 mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa Maji ya Mto Mara Prof.Samuel Manyere kuwaeleze wabunge kilichotokea hali iliyozua mjadala na maswali mengi ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Seleman Jafo alilazimika kutolea ufafanuzi bila mafanikio.
Hata hivyo, ripoti hiyo iliyoonekana kuibua hiasia kwa wabunge imepelekea Balozi wa Mazingira anayewakilisha Bunge, Joseph Kasheku (Musukuma) kujiuzulu nafasi hiyo leo Jumanne Aprili 5, 2022 akisema ni aibu kuwa mwakilishi wakati aliyemteua ameunda ripoti ya hovyo.
Musukuma ambaye ni mbunge wa Geita Vijijini amefikia hatua hiyo baada ya kutofurahishwa na ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha kuchafuka kwa maji ya Mto Mara.
"Ripoti hii hatuitaki. Ni uchafu. Mimi kuanzia leo ninatangaza kujiuzulu ubalozi wa mazingira nilioteuliwa na Waziri Jafo kwa sababu ya mwenendo huu" - Mbunge Musukuma.