Jumatano , 27th Sep , 2023

Wakala wa Nishati vijijini REA watakiwa kuacha tabia ya kutumia muda mrefu kufanya vikao maeneo ya mjini badala yake wafanye vikao na wananchi ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati kwani kazi yao kubwa ni kumaliza changamoto ya ukosefu wa nishati vijijini.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, (wa Nne kutoka kulia) akikata utepe kuashiria umeme kuwashwa. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt Doto Biteko wakati akiwasha  umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Ihako kilichpo wilaya ya Bukombe Mkoani Geita  ambapo ni miongoni mwa vijiji 127 katika mkoa wa Geita vitakavyowashiwa umeme katika mradi wa tatu REA mzunguko wa pili.

“Nawataka REA waende vijijini na tumezungumza siku sio nyingi na nikawambia sasa muda wa kufanya vikao kweny kumbi kubwa huko kwenye makao makuu ya miji huko hatutaki tunataka mwende vijijini nyie ni wakala wa umeme vijijini sio wakala wa umeme mjini vikao vyenu tuone mpo na wananchi magari yenu tuone mnapita humu kwenye vijiji ambapo wanapita wananchi hawa wenye maisha ya kawaida mwende huko mkajifunze lugha yao mfahamu nini wanataka sasa hivi tunaangaika na nishati ya kupikia wananchi wanaoangaika ni wananchi hawa wa chini” Dkt Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Mpaka sasa katika Halmashauri ya wilaya ya Bukombe vimebaki vijiji vitatu ambavyo avijafikiwa na huduma ya nishati ya  umeme, Lutengano Mwalwiba ni Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Bukombe na hapa anabainisha.

“Katika hivi vjiji vitatu vilivyobakia katika hii REA mzunguko wa pili vitakwenda kukamilishwa pia katika hii REA three mzunguko wa pili kuna mradi mwingine unafanyika unaitwa ujazilizwaji yaani Densification kwamba kuna maeneo mengine toka zamani yalikuwa na umeme lakini mengine yaliachwa kwaiyo katika hii awamu yote yatafikiwa” Lutengano Mwalwiba, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

Wananchi wa Kijiji cha Ihako wanaelezea furaha yao baada ya umeme katika eneo hilo kuwashwa rasimi
“Huku kwetu tulikuwa na shida sana saloon tulikuwa hatuna za kunyoa na za kusuka  tulikuwa tunasafiri hadi katome napo ni mbali tunatumia gharama nyingi ila sasa hivi tunashukuru kwa kweli hata chaji ilikuwa ya shida tunatumia sola nayo inamaliza muda mfupi hadi tunakosa mawasiliano kabisa” Chukia Kayogolo Mkazi wa Kijiji cha Ihako

“Kabla ya umeme huu tulikuwa tunapata changamoto kubwa sana kwasasa hivi Tanzania nzima wana vibanda umiza kuonesha mpira kwa sisi wapenzi wa mpira maana betrii ilikuwa inakata moto kabla ya mechi aijaisha lakini kwasasa hilo halijitokezi tena” Emmanuel Mpogoshi Mkazi wa Kijiji cha Ihako

“Yaani tulikuwa tunaishi tunatumia mishumaa,vibatali na sola kwa wenye uwezo lakini tulikuwa tunatumia ghalama kubwa betrii unanunua leo baada ya muda mfupi linaishiwa nguvu inabidi ununue jingine kwaiyo tulikuwa tunatumia ghalama kubwa sana tunaishukuru serikali kwa kutuletea umeme” Gaudensia Kilunga, Mkazi wa Ihako

Aidha serikali  imetoa rai kwa wananchi  wa kijiji hicho kulinda na kuitunza  miundombinu ya umeme iliyopo kijijini hapo.